Jeremiah 42:1-2

Yeremia Ashauri Walionusurika Wasihame Yuda

1 aNdipo maafisa wote wa jeshi, pamoja na Yohanani mwana wa Karea, na Yezania mwana wa Hoshaya, na watu wote kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana wakamjia 2 bYeremia nabii na kumwambia, “Tafadhali sikia maombi yetu na umwombe Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa ajili ya watu hawa wote waliosalia. Kwa kuwa kama unavyoona sasa, ingawa wakati fulani tulikuwa wengi, sasa tumesalia wachache tu.
Copyright information for SwhKC